Soma Biblia Kila Siku 8预览

Pilato akawaambia ... mimi sioni hatia kwake. Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu(m.6-7). Sheria hiyo inasomeka katika Law 24:16:Yeye atakayelikufuru jina la Bwana hakika atauawa! Ajabu yake ni kwamba katika upofu wao Wayahudi wenyewe waliangukia dhambi hiyo ya kumkufuru Mungu! Maana wakadai: Sisi hatuna mfalme ila Kaisari(m.15). Na Wayahudi hawaruhusiwi kamwe kumkiri mfalme mwingine isipokuwa Mungu mwenyewe! Mungu ndiye mfalme wetu pia.