Soma Biblia Kila Siku 8预览

Soma Biblia Kila Siku 8

31天中的第23天

Wayahudi wakamwambia Pilato, Sisi hatuna ruhusa ya kuua mtu. Ili litimie lile neno lake Yesu alilolisema, akionyesha ni mauti gani atakayokufa(m.31-32). Maana yake nini? Wayahudi walikuwa chini ya utawala wa Warumi, na hawakuwa na ruhusa ya kutoa adhabu ya kifo. Njia ya kuadhibu iliyotumika zaidi na Warumi ni kusulibisha, yaani, kumweka mtu juu ya msalaba kwa kumpigilia misumari. Yesu alikwisha tabiri kifo cha aina hii (Yn 3:14: Kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa.Na 12:32-33: Nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu. Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa). Ni mateso makali!

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 8

Soma Biblia Kila Siku 8 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku hasa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kumbukumbu la Torati, na Yohana pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

More