Rukia hadi maudhui

Ruthu 2:7 - Linganisha Matoleo Yote

Ruthu 2:7 BHN (Biblia Habari Njema)

Aliniomba nimruhusu awafuate nyuma wavunaji huku akiokota masazo kati ya miganda. Basi alikuja na amefanya kazi tangu asubuhi na ni sasa tu amekwenda kupumzika kibandani.”

Ruthu 2 BHN

Ruthu 2:7 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

naye akasema, Tafadhali niruhusu kuokota masazo, na kukusanya nyuma ya wavunaji kati ya miganda; basi akaja, naye ameshinda tangu asubuhi hata sasa, isipokuwa alikaa nyumbani kitambo kidogo.

Ruthu 2 SUV

Ruthu 2:7 SRUV (Swahili Revised Union Version)

naye akasema, Tafadhali niruhusu kuokota mabaki, na kukusanya nyuma ya wavunaji kati ya miganda; basi akaja, naye ameshinda tangu asubuhi hadi sasa, isipokuwa alikaa nyumbani kitambo kidogo.

Ruthu 2 SRUV

Ruthu 2:7 NEN (Neno)

Yeye aliomba, ‘Tafadhali niruhusu niokote na kukusanya miongoni mwa miganda nyuma ya wavunaji.’ Naye ameshinda shambani tangu asubuhi pasipo kupumzika, isipokuwa kwa muda mfupi kivulini.”

Ruthu 2 NEN