Waroma 15:9 - Linganisha Matoleo Yote
Waroma 15:9 BHN (Biblia Habari Njema)
ili nao watu wa mataifa mengine wapate kumtukuza Mungu kwa sababu ya huruma yake. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Kwa hiyo nitakusifu miongoni mwa watu wa mataifa. Nitaziimba sifa za jina lako.”
Waroma 15:9 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa, Nami nitaliimbia jina lako.
Waroma 15:9 SRUV (Swahili Revised Union Version)
tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa, Nami nitaliimbia jina lako.
Waroma 15:9 NEN (Neno)
na pia ili watu wa Mataifa wamtukuze Mungu kwa rehema zake. Kama ilivyoandikwa: “Kwa hiyo nitakutukuza kati ya watu wa Mataifa; nitaliimbia sifa jina lako.”