Rukia hadi maudhui

Waroma 15:27 - Linganisha Matoleo Yote

Waroma 15:27 BHN (Biblia Habari Njema)

Wao wenyewe wameamua kufanya hivyo; lakini, kwa kweli, hilo ni jukumu lao kwa hao. Maana, ikiwa watu wa mataifa mengine wameshiriki baraka za kiroho za Wayahudi, wanapaswa nao pia kuwahudumia Wayahudi katika mahitaji yao ya kidunia.

Waroma 15 BHN

Waroma 15:27 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Naam, imewapendeza, tena wamekuwa wadeni wao. Kwa maana ikiwa Mataifa wameyashiriki mambo yao ya roho, imewabidi kuwahudumu kwa mambo yao ya mwili.

Waroma 15 SUV

Waroma 15:27 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Naam, imewapendeza, tena wamekuwa wadeni wao. Kwa maana ikiwa Mataifa wameyashiriki mambo yao ya roho, imewabidi kuwahudumia kwa mambo yao ya mwili.

Waroma 15 SRUV

Waroma 15:27 NEN (Neno)

Imewapendeza kufanya hivyo, naam, kwani ni wadeni wao. Kwa maana ikiwa watu wa Mataifa wameshiriki baraka za rohoni za Wayahudi, wao ni wadeni wa Wayahudi, ili Wayahudi nao washiriki baraka zao za mambo ya mwilini.

Waroma 15 NEN