Hesabu 27:4 - Linganisha Matoleo Yote
Hesabu 27:4 BHN (Biblia Habari Njema)
Yeye hakuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora waliokusanyika dhidi ya Mwenyezi-Mungu, bali alikufa kutokana na dhambi yake mwenyewe. Kwa nini basi jina la baba yetu lifutwe katika ukoo wake kwa sababu hakuwa na mtoto wa kiume? Tupe urithi pamoja na ndugu zake baba yetu.”
Hesabu 27:4 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa nini basi jina la babaetu kufutwa katika jamaa zake kwa sababu alikuwa hana mwana wa kiume? Tupe sisi urithi pamoja na ndugu zake babaetu.
Hesabu 27:4 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Kwa nini basi jina la baba yetu kufutwa katika jamaa zake kwa sababu alikuwa hana mwana wa kiume? Tupe sisi urithi pamoja na ndugu zake baba yetu.
Hesabu 27:4 NEN (Neno)
Kwa nini jina la baba yetu lifutike kutoka ukoo wake kwa sababu hakuwa na mwana? Tupatie milki miongoni mwa ndugu za baba yetu.”