Hesabu 2:31 - Linganisha Matoleo Yote
Hesabu 2:31 BHN (Biblia Habari Njema)
Jumla ya watu watakaokuwa katika kambi ya Dani kulingana na makundi yao ni watu 157,600. Kundi hili la Dani litakuwa katika msafara wa mwisho, bendera baada ya bendera.”
Hesabu 2:31 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wote waliohesabiwa katika marago ya Dani walikuwa mia na hamsini na saba elfu na mia sita. Hao ndio watakaosafiri mwisho kwa kuandama beramu zao.
Hesabu 2:31 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Wote waliohesabiwa katika kambi ya Dani walikuwa elfu mia moja hamsini na saba na mia sita. Hao ndio watakaoondoka mwisho kwa kufuata bendera yao.
Hesabu 2:31 NEN (Neno)
Wanaume wote walio katika kambi ya Dani ni elfu mia moja hamsini na saba na mia sita. Wao watakuwa wa mwisho kuondoka chini ya beramu yao.