Rukia hadi maudhui

Hesabu 19:2 - Linganisha Matoleo Yote

Hesabu 19:2 BHN (Biblia Habari Njema)

“Haya ni masharti ya sheria ambayo mimi Mwenyezi-Mungu ninatoa. Waambieni Waisraeli wawaletee ng'ombe jike mwekundu asiye na dosari wala kasoro yoyote, na ambaye hajapata kufungwa nira.

Hesabu 19 BHN

Hesabu 19:2 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Hii ndiyo amri ya sheria BWANA aliyoagiza, akisema, Waambie wana wa Israeli wakuletee ng’ombe mke mwekundu asiye na kipaku, mkamilifu, ambaye hajatiwa nira bado

Hesabu 19 SUV

Hesabu 19:2 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Hii ndiyo amri ya sheria BWANA aliyoagiza, akisema, Waambie wana wa Israeli wakuletee ng'ombe jike mwekundu asiye na doa, mkamilifu, ambaye hajatiwa nira bado

Hesabu 19 SRUV

Hesabu 19:2 NEN (Neno)

“Hivi ndivyo sheria ambayo BWANA ameagiza itakavyo: Waambie Waisraeli wakuletee mtamba mwekundu asiye na dosari wala waa, na ambaye hajapata kufungwa nira.

Hesabu 19 NEN