Mika 2:2 - Linganisha Matoleo Yote
Mika 2:2 BHN (Biblia Habari Njema)
Hutamani mashamba na kuyatwaa; wakitaka nyumba, wananyakua. Huwadhulumu wenye nyumba na jamaa zao, huwanyang'anya watu mali zao.
Mika 2:2 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao hutamani mashamba, na kuyashika; na nyumba pia, nao huzichukua; nao humwonea mtu na nyumba yake, naam, mtu na urithi wake.
Mika 2:2 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Nao hutamani mashamba, na kuyanyakua; na nyumba pia, nao huzichukua; nao humwonea mtu na nyumba yake, naam, mtu na urithi wake.
Mika 2:2 NEN (Neno)
Wanatamani mashamba na kuyakamata, pia nyumba na kuzichukua. Wanamlaghai mwanaume nyumba yake, mwanadamu mwenzake urithi wake.