Nembo ya Programu ya Biblia
Ikoni ya Utafutaji

Walawi 7:35-36 - Linganisha Matoleo Yote

Walawi 7:35-36 BHN (Biblia Habari Njema)

Hiyo ndiyo sehemu iliyotengwa kwa ajili ya Aroni na wanawe kutoka katika sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto, tangu siku walipotawazwa kuwa makuhani wa Mwenyezi-Mungu. Walipowekwa wakfu kwa kupakwa mafuta, Mwenyezi-Mungu aliamuru Waisraeli wawape sehemu hiyo ya sadaka; hiyo itakuwa daima haki yao.”

Shirikisha
Walawi 7 BHN

Walawi 7:35-36 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Hii ndiyo sehemu ya Haruni, na sehemu ya wanawe, katika kutiwa mafuta kwao, katika hizo dhabihu zisongezwazo kwa BWANA kwa njia ya moto, siku hiyo aliyowaweka ili wamtumikie BWANA katika kazi ya ukuhani; sehemu ambayo BWANA aliagiza wapewe na wana wa Israeli, siku hiyo aliyowatia mafuta. Ni haki yao ya milele katika vizazi vyao vyote.

Shirikisha
Walawi 7 SUV

Walawi 7:35-36 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Hii ndiyo sehemu ya Haruni, na sehemu ya wanawe, katika kutiwa mafuta kwao, katika hizo dhabihu zisongezwazo kwa BWANA kwa njia ya moto, siku hiyo aliyowaweka ili wamtumikie BWANA katika kazi ya ukuhani; sehemu ambayo BWANA aliagiza wapewe na wana wa Israeli, siku hiyo aliyowatia mafuta. Ni haki yao ya milele katika vizazi vyao vyote.

Shirikisha
Walawi 7 SRUV

Walawi 7:35-36 NEN (Neno)

Hii ndiyo sehemu ya sadaka zilizotolewa kwa BWANA kwa moto, ambazo zilitengwa kwa ajili ya Haruni na wanawe siku ile walipowekwa wakfu ili kumtumikia BWANA katika kazi ya ukuhani. Siku ile walipopakwa mafuta, BWANA aliagiza kwamba Waisraeli wawape hili kama fungu lao la milele kwa vizazi vijavyo.

Shirikisha
Walawi 7 NEN