Yoshua 7:26 - Linganisha Matoleo Yote
Yoshua 7:26 BHN (Biblia Habari Njema)
Halafu wakarundika mawe mengi juu yake, ambayo yako hadi leo. Hapo hasira ya Mwenyezi-Mungu ikapoa; na mahali hapo pakaitwa Bonde la Akori mpaka hivi leo.
Yoshua 7:26 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha wakakusanya juu yake chungu kubwa ya mawe hata leo; naye BWANA akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde la Akori, hata hivi leo.
Yoshua 7:26 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Kisha wakakusanya juu yake rundo kubwa la mawe hata leo; naye BWANA akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde la Akori, hata leo.
Yoshua 7:26 NEN (Neno)
Wakakusanya lundo la mawe juu ya Akani, ambalo lipo hadi leo. Naye BWANA akageuka kutoka hasira yake kali. Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Bonde la Akori tangu siku hiyo.