Hosea 2:2 - Linganisha Matoleo Yote
Hosea 2:2 BHN (Biblia Habari Njema)
Mlaumuni mama yenu mlaumuni, maana sasa yeye si mke wangu wala mimi si mume wake. Mlaumuni aondokane na uasherati wake, ajiepushe na uzinzi wake.
Shirikisha
Hosea 2 BHNHosea 2:2 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Msihini mama yenu, msihini; kwa maana yeye si mke wangu, wala mimi si mume wake; na ayawekee mbali mambo ya uasherati wake yasiwe mbele ya uso wake, na mambo ya uzinzi wake yasiwe kati ya maziwa yake
Shirikisha
Hosea 2 SUVHosea 2:2 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Msihini mama yenu, msihini; kwa maana yeye si mke wangu, wala mimi si mume wake; na aondokane na usherati wake usiwe mbele ya uso wake, na uzinzi wake usiwe kati ya matiti yake
Shirikisha
Hosea 2 SRUVHosea 2:2 NEN (Neno)
“Mkemeeni mama yenu, mkemeeni, kwa maana yeye si mke wangu, nami si mume wake. Aondoe sura ya uzinzi katika uso wake na uzinzi kati ya matiti yake.
Shirikisha
Hosea 2 NEN