Esta 9:3 - Linganisha Matoleo Yote
Esta 9:3 BHN (Biblia Habari Njema)
Ikawa viongozi wote wa mikoa, watawala, wakuu na maofisa wa mfalme pia waliwasaidia Wayahudi, maana wote walimwogopa Mordekai.
Esta 9:3 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao maakida wa majimbo, na majumbe, na maliwali, na wale waliofanya shughuli ya mfalme, waliwasaidia Wayahudi; kwa sababu hofu ya Mordekai imewaangukia.
Esta 9:3 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Nao wakuu wa mikoa, na majumbe, na watawala, na wale waliofanya shughuli ya mfalme, waliwasaidia Wayahudi; maana walimwogopa Mordekai.
Esta 9:3 NEN (Neno)
Nao wakuu wote wa majimbo, majemadari, watawala na maafisa wa mfalme wakawasaidia Wayahudi, kwa sababu walimhofu Mordekai.