Rukia hadi maudhui

Esta 7:4 - Linganisha Matoleo Yote

Esta 7:4 BHN (Biblia Habari Njema)

Maana, mimi na watu wangu tumeuzwa tuuawe, kuangamizwa na kufutiliwa mbali. Kama tungeuzwa tu kuwa watumwa na watumwa wa kike, ningekaa kimya, wala nisingekusumbua. Ingawa tutakatiliwa mbali hakuna adui atakayeweza kufidia hasara hii kwa mfalme.”

Esta 7 BHN

Esta 7:4 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Maana tumeuzwa, mimi na watu wangu, ili tuharibiwe, na kuuawa, na kuangamia. Kama tungaliuzwa kuwa watumwa na wajakazi, ningalinyamaza; ila hata hivyo msiba wetu haulinganishwi na hasara ya mfalme.

Esta 7 SUV

Esta 7:4 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Maana tumeuzwa, mimi na watu wangu, ili tuharibiwe, na kuuawa, na kuangamia. Kama tungaliuzwa kuwa watumwa na wajakazi, ningalinyamaza; japo hata hivyo adui asingeweza kufidia hasara ya mfalme.

Esta 7 SRUV

Esta 7:4 NEN (Neno)

Kwa kuwa mimi na watu wangu tumeuzwa ili tuangamizwe, tuchinjwe na tuharibiwe. Tungeuzwa tu kama watumwa wa kiume na wa kike, ningenyamaza, kwa sababu shida kiasi hicho haingetosha kumsumbua mfalme.”

Esta 7 NEN