Rukia hadi maudhui

Esta 6:4 - Linganisha Matoleo Yote

Esta 6:4 BHN (Biblia Habari Njema)

Mfalme akauliza, “Kuna ofisa yeyote uani?” Ikawa wakati huo Hamani alikuwa ameingia katika ua wa nje wa ikulu; alikuwa amekuja kwa mfalme kuomba Mordekai auawe kwenye mti wa kuulia ambao alikuwa amekwisha mtayarishia.

Esta 6 BHN

Esta 6:4 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Mfalme akasema, Yupo nani behewani? Ikawa Hamani alikuwa ameingia katika ua wa nje wa nyumba ya mfalme, aseme na mfalme, ili kumtundika Mordekai juu ya mti ule aliomwekea tayari.

Esta 6 SUV

Esta 6:4 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Mfalme akasema, Yupo nani behewani? Ikawa Hamani alikuwa ameingia katika ua wa nje wa nyumba ya mfalme, aseme na mfalme, ili kumtundika Mordekai juu ya mti ule aliomwandalia.

Esta 6 SRUV

Esta 6:4 NEN (Neno)

Mfalme akasema, “Ni nani yuko uani?” Wakati huo huo Hamani alikuwa ameingia kwenye ua wa nje wa jumba la mfalme kusema na mfalme kuhusu kumwangika Mordekai katika mahali pa kuangikia watu alipokuwa amepajenga kwa ajili yake.

Esta 6 NEN