Skip to content

Esta 4:3 - Linganisha Matoleo Yote

Esta 4:3 BHN (Biblia Habari Njema)

Katika kila mkoa, mara tu amri ya mfalme ilipotangazwa, msiba mkubwa uliwakumba Wayahudi. Walifunga, wakalia na kuomboleza; na wengi wao walilala katika majivu wakiwa wamevaa magunia.

Esta 4 BHN

Esta 4:3 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Na katika kila jimbo, ambako amri ya mfalme na mbiu yake imewasili, palikuwako msiba mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu.

Esta 4 SUV

Esta 4:3 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Na katika kila mkoa, ambako amri ya mfalme na mbiu yake imewasili, palikuwako msiba mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu.

Esta 4 SRUV

Esta 4:3 NEN (Neno)

Katika kila jimbo ambapo amri na agizo la mfalme lilifika, kulikuwa na maombolezo makuu miongoni mwa Wayahudi pamoja na kufunga, kulia na kuomboleza. Watu wengi wakalala juu ya magunia na majivu.

Esta 4 NEN