Esta 4:1 - Linganisha Matoleo Yote
Esta 4:1 BHN (Biblia Habari Njema)
Mordekai alipojua yote yaliyotukia, alizirarua nguo zake, akavaa vazi la gunia, na kujitia majivu. Kisha, akapita katikati ya mji akilia kwa sauti ya uchungu.
Esta 4:1 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Mordeikai alipojua mambo yote yaliyofanyika, alizirarua nguo zake, akajivika gunia pamoja na majivu, akatoka hata kufika katikati ya mji, akalia kwa sauti kuu ya uchungu.
Esta 4:1 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Basi Mordekai alipojua mambo yote yaliyofanyika, alizirarua nguo zake, akajivika gunia na kujipaka majivu, akatoka hadi katikati ya mji, akalia kwa sauti kuu ya uchungu.
Esta 4:1 NEN (Neno)
Mordekai alipojua yote yaliyokwisha kufanyika, alirarua mavazi yake, akavaa magunia na kujipaka majivu, akaenda mjini akiomboleza kwa sauti na kwa uchungu.