Esta 2:18 - Linganisha Matoleo Yote
Esta 2:18 BHN (Biblia Habari Njema)
Kisha mfalme akaandaa karamu kubwa kwa heshima ya Esta, akawaalika viongozi na watumishi wote wa serikali yake. Pia, mfalme alitangaza msamaha wa kodi katika mikoa yote, akatoa zawadi nyingi kulingana na hadhi yake ya kifalme.
Esta 2:18 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo mfalme alipowafanyia karamu kubwa maakida wake wote na watumishi wake, yaani, karamu yake Esta; akafanya msamaha katika majimbo yote, akatoa zawadi sawasawa na ukarimu wa mfalme.
Esta 2:18 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Ndipo mfalme alipowafanyia karamu kubwa wakuu wake wote na watumishi wake, yaani, karamu yake Esta; akafanya msamaha katika majimbo yote, akatoa zawadi kulingana na ukarimu wa mfalme.
Esta 2:18 NEN (Neno)
Mfalme akafanya karamu kubwa, karamu ya Esta, kwa wakuu wake wote na maafisa. Mfalme akatangaza siku ya mapumziko katika majimbo yake yote na kugawa zawadi kwa ukarimu wa kifalme.