Danieli 6:3 - Linganisha Matoleo Yote
Danieli 6:3 BHN (Biblia Habari Njema)
Muda si muda, Danieli akadhihirika kuwa bora kuliko wale wasimamizi wengine na wakuu wote kwa kuwa alikuwa na roho njema. Hivyo mfalme akanuia kumpa uongozi wa ufalme wote.
Shirikisha
Danieli 6 BHNDanieli 6:3 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.
Shirikisha
Danieli 6 SUVDanieli 6:3 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na watawala, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.
Shirikisha
Danieli 6 SRUVDanieli 6:3 NEN (Neno)
Basi Danieli alijidhihirisha miongoni mwa wasimamizi na wakuu kwa sifa zake za kipekee, hata mfalme akapanga kumweka juu ya ufalme wote.
Shirikisha
Danieli 6 NEN