Danieli 6:1-2 - Linganisha Matoleo Yote
Danieli 6:1-2 BHN (Biblia Habari Njema)
Mfalme Dario aliamua kuteua wakuu 120 kusimamia mambo ya utawala. Aliwateua pia wakuu watatu, Danieli akiwa mmojawapo, wawasimamie wale wakuu wengine na maslahi ya mfalme, asije akapata hasara.
Danieli 6:1-2 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote; na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara.
Danieli 6:1-2 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme wakuu mia moja na ishirini, wawe juu ya ufalme wote; na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili wakuu hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara.
Danieli 6:1-2 NEN (Neno)
Ilimpendeza Dario kuteua wakuu mia moja na ishirini kutawala katika ufalme wake wote, pamoja na wasimamizi watatu juu yao, Danieli akiwa mmoja wao. Wakuu walitoa hesabu kwa wasimamizi hao ili mfalme asipate hasara.