Matendo 8:32 - Linganisha Matoleo Yote
Matendo 8:32 BHN (Biblia Habari Njema)
Basi, sehemu ya Maandiko Matakatifu aliyokuwa anasoma ilikuwa hii: “Alikuwa kama kondoo anayepelekwa kuchinjwa; kimya kama vile mwanakondoo anapokatwa manyoya, yeye hakutoa sauti hata kidogo.
Matendo 8:32 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.
Matendo 8:32 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake yule amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.
Matendo 8:32 NEN (Neno)
Huyu towashi alikuwa anasoma fungu hili la Maandiko: “Aliongozwa kama kondoo aendaye machinjoni, kama mwana-kondoo anyamazavyo mbele yake yule amkataye manyoya, hivyo hakufungua kinywa chake.