Rukia hadi maudhui

Matendo 8:27 - Linganisha Matoleo Yote

Matendo 8:27 BHN (Biblia Habari Njema)

Basi, Filipo akajiweka tayari, akaanza safari. Wakati huohuo kulikuwa na Mwethiopia mmoja, towashi, ambaye alikuwa anasafiri kuelekea nyumbani. Huyo mtu alikuwa mkurugenzi maarufu wa hazina ya Kandake, malkia wa Ethiopia. Alikuwa amekwenda huko Yerusalemu kuabudu na wakati huo alikuwa anarudi akiwa amepanda gari la kukokotwa.

Matendo 8 BHN

Matendo 8:27 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu

Matendo 8 SUV

Matendo 8:27 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyesimamia hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu

Matendo 8 SRUV

Matendo 8:27 NEN (Neno)

Hivyo akaondoka. Akiwa njiani akakutana na towashi wa Kushi, aliyekuwa afisa mkuu, mwenye mamlaka juu ya hazina zote za Kandake, Malkia wa Kushi. Huyu towashi alikuwa ameenda Yerusalemu ili kuabudu

Matendo 8 NEN