Matendo 7:8 - Linganisha Matoleo Yote
Matendo 7:8 BHN (Biblia Habari Njema)
Halafu Mungu akafanya naye agano ambalo tohara ni ishara yake. Hivyo, Abrahamu alimtahiri mtoto wake Isaka siku ya nane baada ya kuzaliwa. Na Isaka, vivyo hivyo, alimtahiri Yakobo. Naye Yakobo aliwatendea wale mababu kumi na wawili vivyo hivyo.
Shirikisha
Matendo 7 BHNMatendo 7:8 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akampa agano la tohara; basi Ibrahimu akamzaa Isaka, akamtahiri siku ya nane. Isaka akamzaa Yakobo. Yakobo akawazaa wale kumi na wawili, wazee wetu.
Shirikisha
Matendo 7 SUVMatendo 7:8 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Akampa agano la tohara; basi Abrahamu akamzaa Isaka, akamtahiri siku ya nane. Isaka akamzaa Yakobo. Yakobo akawazaa wale kumi na wawili, wazee wetu.
Shirikisha
Matendo 7 SRUVMatendo 7:8 NEN (Neno)
Ndipo akampa Abrahamu agano la tohara. Naye Abrahamu akamzaa Isaka na kumtahiri siku ya nane. Baadaye Isaka akamzaa Yakobo, naye Yakobo akawazaa wale baba zetu wa zamani kumi na wawili.
Shirikisha
Matendo 7 NEN