Matendo 7:42 - Linganisha Matoleo Yote
Matendo 7:42 BHN (Biblia Habari Njema)
Lakini Mungu aliondoka kati yao, akawaacha waabudu nyota za anga, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii: ‘Enyi watu wa Israeli! Si mimi mliyenitolea tambiko na sadaka kwa miaka arubaini kule jangwani!
Matendo 7:42 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii, Je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka Miaka arobaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?
Matendo 7:42 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii, Je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka Miaka arubaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?
Matendo 7:42 NEN (Neno)
Ndipo Mungu akageuka, akawaachia waabudu jeshi lote la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Manabii: “ ‘Je, mliniletea dhabihu na sadaka kwa miaka arobaini kule jangwani, ee nyumba ya Israeli?