Rukia hadi maudhui

Matendo 5:36 - Linganisha Matoleo Yote

Matendo 5:36 BHN (Biblia Habari Njema)

Zamani kidogo, kulitokea mtu mmoja jina lake Theuda, akajisema kuwa mtu wa maana na watu karibu 400 wakajiunga naye. Lakini aliuawa, kisha wafuasi wake wote wakatawanyika na kikundi chake kikafa.

Matendo 5 BHN

Matendo 5:36 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akijidai ya kuwa yeye ni mtu mkuu, watu wapata mia nne wakashikamana naye; naye aliuawa na wote waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu.

Matendo 5 SUV

Matendo 5:36 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akijidai ya kuwa yeye ni mtu mkuu, watu wapatao mia nne wakashikamana naye; naye aliuawa na wote waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu.

Matendo 5 SRUV

Matendo 5:36 NEN (Neno)

Kwa maana wakati uliopita, aliinuka mtu mmoja jina lake Theuda, alijidai kuwa yeye ni mtu maarufu, akapata wafuasi wapatao mia nne walioambatana naye. Lakini aliuawa, na wafuasi wake wote wakatawanyika, wakawa si kitu.

Matendo 5 NEN