Rukia hadi maudhui

Matendo 27:7 - Linganisha Matoleo Yote

Matendo 27:7 BHN (Biblia Habari Njema)

Kwa muda wa siku nyingi tulisafiri polepole, na kwa shida tulifika karibu na Nido. Kwa sababu upepo ulikuwa bado unatupinga, tuliendelea mbele moja kwa moja tukapitia upande wa Krete karibu na rasi Salmone ambapo upepo haukuwa mwingi.

Matendo 27 BHN

Matendo 27:7 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Tukasafiri polepole kwa muda wa siku nyingi, tukafika mpaka Nido kwa shida; na kwa sababu upepo ulikuwa ukituzuia tukapita chini ya Krete, tukaikabili Salmone.

Matendo 27 SUV

Matendo 27:7 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Tukasafiri polepole kwa muda wa siku nyingi, tukafika mpaka Nido kwa shida; na kwa sababu upepo ulikuwa ukituzuia tukapita chini ya Krete, tukaikabili Salmone.

Matendo 27 SRUV

Matendo 27:7 NEN (Neno)

Tukasafiri polepole kwa siku nyingi na kwa shida, hatimaye tukafika karibu na Nido. Kwa kuwa upepo wa mbisho ulituzuia tusiweze kushika mwelekeo tuliokusudia, tukapita chini ya Krete mkabala na Salmone.

Matendo 27 NEN