Matendo 17:22 - Linganisha Matoleo Yote
Matendo 17:22 BHN (Biblia Habari Njema)
Basi, Paulo alisimama mbele ya baraza la Areopago, akasema, “Wananchi wa Athene! Ninaona kwamba nyinyi, kwa vyovyote, ni watu wa dini sana
Matendo 17:22 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema, Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini.
Matendo 17:22 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema, Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini.
Matendo 17:22 NEN (Neno)
Ndipo Paulo akasimama katikati ya mkutano wa Areopago, akasema, “Enyi watu wa Athene! Ninaona kwamba katika kila jambo ninyi ni watu wa dini sana.