Matendo 16:19 - Linganisha Matoleo Yote
Matendo 16:19 BHN (Biblia Habari Njema)
Matajiri wa yule msichana walipoona kwamba tumaini lao la kupata mali limekwisha, waliwakamata Paulo na Sila, wakawaburuta mpaka hadharani, mbele ya wakuu.
Matendo 16:19 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji
Matendo 16:19 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Basi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji
Matendo 16:19 NEN (Neno)
Basi mabwana wa yule mjakazi walipoona kuwa tumaini lao la kuendelea kujipatia fedha limetoweka, wakawakamata Paulo na Sila wakawaburuta hadi sokoni mbele ya viongozi wa mji.