Zaburi 95
95
Zaburi 95
Wimbo wa kumsifu Mungu
1 Njooni, tumwimbie Bwana kwa furaha;
tumfanyie kelele za shangwe
Mwamba wa wokovu wetu.
2 Tuje mbele zake kwa shukrani,
tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.
3 Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu,
mfalme mkuu juu ya miungu yote.
4 Mkononi mwake mna vilindi vya dunia,
na vilele vya milima ni mali yake.
5 Bahari ni yake, kwani ndiye aliyeifanya,
na mikono yake iliumba nchi kavu.
6 Njooni, tusujudu, tumwabudu,
tupige magoti mbele za Bwana Muumba wetu,
7 kwa maana yeye ndiye Mungu wetu,
na sisi ni watu wa malisho yake,
kondoo chini ya utunzaji wake.
Mkiisikia sauti yake leo,
8 msiifanye mioyo yenu migumu
kama mlivyofanya kule Meriba#95:8 maana yake Kugombana,
kama mlivyofanya siku ile
kule Masa#95:8 maana yake Kujaribiwa jangwani,
9 ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima,
ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu.
10 Kwa miaka arobaini nilikasirikia kizazi kile,
nikasema, “Hawa ni taifa ambalo mioyo yao imepotoka,
nao hawajazijua njia zangu.”
11 Hivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu,
“Kamwe hawataingia rahani mwangu.”
Selectat acum:
Zaburi 95: NEN
Evidențiere
Copiază
Compară
Împărtășește
Dorești să ai evidențierile salvate pe toate dispozitivele? Înscrie-te sau conectează-te
Holy Bible, Kiswahili Contemporary Version™ (Neno: Biblia Takatifu™) | Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. | Used with permission. All rights reserved worldwide.
Biblica® Cross Reference System | Copyright © 2025 by Biblica, Inc. | Used with permission. All rights reserved worldwide.