YouVersion Logo
Search Icon

Mhubiri UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu cha Mhubiri (Kiebrania: “Kohelethi”, Kilatini: “Eklesiastes”) kina mawaidha ya mtu ambaye alitafakari sana juu ya ufupi wa maisha ya mwanadamu na mambo yake ya kutatiza, akachunguza na falsafa yake, akayaona hayo yote kuwa magumu yasiyoeleweka: “Kila kitu ni bure kabisa”. Katika huko kuwaza na kuwazua kwake anaona kwamba haiwezekani kuelewa mipango ya Mungu ambaye anaongoza mambo duniani. Hata hivyo anawahimiza watu wafanye kazi kwa bidii na kufurahia vipaji walivyopewa na Mungu muda wote waishipo.
Mwandishi: Hatuna mengi ya kuweza kumtambulisha ila ianaonekana kwamba alikuwa mmojawapo wa watu wenye hekima nyakati za utamaduni wa Kigiriki katika Mashariki ya kati ya Kale. Alikuwa mtu mwenye kufikiri sana na ambaye hakutosheka tu na kurudiarudia mawazo na mapokeo ya nyakati zake. Ingawa anamtaja mfalme Solomoni “mwana wa Daudi, mfalme huko Yerusalemu” (1:1,12) na pia anaposema juu ya kazi na utajiri wake (2:4-9), mambo anayoyazungumzia ni ya wakati wa baadaye sana.
Fikira nyingi za Mhubiri huyu zaonekana kuwa za kutatiza na za mashaka. Hata hivyo anao msimamo wa kidini na anatushauri mwishoni: “Mche Mungu, na uzishike amri zake; kwa sababu hilo ndilo jukumu aliloumbiwa mwanadamu” (12:13).

Currently Selected:

Mhubiri UTANGULIZI: BHND

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy