YouVersion Logo
Search Icon

2 Mambo ya Nyakati UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu hiki cha pili cha Mambo ya Nyakati kinaendeleza masimulizi yale yaliyoachwa na kile cha kwanza; kinaanza kwa kueleza utawala wa Solomoni mpaka kufa kwake. Baada ya kusimulia juu ya uasi wa utawala wa makabila ya kaskazini chini ya Yeroboamu dhidi ya Rehoboamu mwanawe mfalme Solomoni na ambaye alitawala baada yake, kitabu kinaendelea hasa kusimulia habari za ufalme wa kusini wa Yuda mpaka wakati wa kuharibiwa mji wa Yerusalemu mnamo mwaka 586 K.K.
Aya za mwisho za kitabu hiki zinahusiana na vitabu vya Ezra na Nehemia na zinatualika kuendelea kusoma historia ya watu wa Israeli. Yamkini hapa mwishoni pana maneno yanayokariri tangazo alilotoa mfalme Koreshi ambalo liliwaruhusu Wayahudi kurudi makwao na kujenga upya hekalu la Yerusalemu. Tangazo hilohilo limeandikwa lote mwanzoni mwa kitabu cha Ezra.

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy