YouVersion Logo
Search Icon

1 Wamakabayo UTANGULIZI

UTANGULIZI
Vitabu vya Makabayo vimepewa jina alilopewa mtu ambaye anahusika zaidi katika masimulizi yake, yaani, Yuda, na ambalo walipewa pia nduguze: Yonathani na Simoni. Hapa tunapewa historia ya Wayahudi mnamo mwaka 187-142 K.K. Historia hiyo aghalabu ni juu ya mapambano ya baadhi ya Wayahudi ya kujipatia uhuru wa kisiasa na kidini.
Kitabu cha kwanza ambacho yaonekana kwamba kilifasiriwa katika Kigiriki kutoka makala ya awali ya Kiebrania ambayo haikuhifadhiwa, chahusika na wakati wa miaka ya 175-134 K.K. Huo ulikuwa wakati wa mfalme Aleksanda Mkuu na wafalme waliofuata baada yake wajulikanao kwa jumla kama wafalme Waseleuko, wakati wa siasa ya Antioko ambayo iliwashurutisha Wayahudi kufuata desturi na ibada za mila ya Kigiriki. Ukatili wa siasa hiyo ya Antioko ndio uliosababisha uasi wa kuhani Matathia na wanawe (sura 1).
Yuda Makabayo anaongoza mapambano ya silaha dhidi ya makamanda wa jeshi la Waseleuko: Lusia, Bakide na Nikanori (Sura 2:1–9:22). Baada ya kifo chake Yuda, ndugu yake Yonathani anaendeleza mapambano hayo, lakini mapambano yake yalikuwa ya kisiasa zaidi kuliko ya silaha. Huyu Yonathani alifanywa kuwa kuhani mkuu na mfalme Aleksanda Bala, lakini aliuawa mnamo mwaka 142 (9:23–12:53). Yonathani alifuatwa na nduguye Simoni (142-134). Huyu naye aliteuliwa kuwa kuhani mkuu na mfalme Demetrio II, akafufua yale mapambano ya silaha, na kuwapatia wananchi wenzake madaraka. Huyu Simoni Makabayo ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa ukoo wa Wahasmoneo (13-16).

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy