YouVersion Logo
Search Icon

Zek 2

2
Maono ya Tatu: Mtu Mwenye Kamba ya Kupima
1 # Eze 40:3; Zek 1:16 Kisha nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake. 2#Ufu 11:1Ndipo nikasema, Unakwenda wapi? Akaniambia, Ninakwenda kuupima Yerusalemu, nione upana wake ulivyo na urefu wake ulivyo. 3Na tazama, yule malaika aliyesema nami akasimama karibu, na malaika mwingine akatoka ili kuonana naye; 4#Eze 36:10naye akamwambia, Piga mbio, kamwambie kijana huyu, na kusema, Yerusalemu utakaliwa na watu, kama vijiji visivyo na kuta, kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo ndani yake. 5#Zab 46:11; Isa 4:5; Ufu 21:23Kwa maana mimi, asema BWANA, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.
Mapumziko: Mwito kwa Waliohamishwa
6 # Kum 28:64 Haya! Haya! Ikimbieni nchi ya kaskazini, asema BWANA; kwa maana mimi nimewatawanya ninyi kama pepo nne za mbinguni, asema BWANA. 7Haya! Ee Sayuni, jiponye, wewe ukaaye pamoja na binti Babeli. 8#2 The 1:6Kwa maana BWANA wa majeshi asema hivi, Ili nitafute utukufu amenituma kwa mataifa wale waliowateka ninyi; maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho lake. 9Kwa maana, tazama, nitatikisa mkono wangu juu yao, nao watakuwa mateka ya hao waliowatumikia; nanyi mtajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma. 10#Law 26:12; 2 Kor 6:16Imba, ufurahi, Ee binti Sayuni; maana, tazama, ninakuja, nami nitakaa kati yako, asema BWANA. 11#Isa 2:2,3; Kut 12:49; Eze 33:33Na mataifa mengi watajiunga na BWANA katika siku ile, nao watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwako. 12#Kum 32:9Na BWANA atairithi Yuda, iwe sehemu yake katika nchi takatifu, naye atachagua Yerusalemu tena. 13#Zab 46:10; Hab 2:20; Rum 3:19Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za BWANA; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu.

Currently Selected:

Zek 2: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy