YouVersion Logo
Search Icon

Neh 3

3
Utaratibu wa Kazi
1 # Neh 12:10,39; Yn 5:2; Yer 31:38; Zek 14:10 Ndipo akaondoka Eliashibu, kuhani mkuu, pamoja na nduguze makuhani, wakalijenga lango la kondoo; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake; mpaka mnara wa Hamea wakalitakasa, mpaka mnara wa Hananeli. 2#Ezr 2:34; Neh 7:36Na baada yao wakajenga watu wa Yeriko. Na baada yao akajenga Zakuri, mwana wa Imri. 3#2 Nya 33:14; Neh 12:39; Sef 1:10; Neh 6:1Na lango la samaki wakalijenga wana wa Senaa; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake. 4Na baada yao akafanyiza Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi. Na baada yao akafanyiza Meshulamu, mwana wa Berekia, mwana wa Meshezabeli. Na baada yao akafanyiza Sadoki, mwana wa Baana. 5#Amu 5:23Na baada yao wakafanyiza Watekoi; lakini wakuu wao hawakutia shingo zao kazini mwa bwana wao. 6#Neh 12:39Na lango la kale wakalifanyiza Yoyada, mwana wa Pasea, na Meshulamu, mwana wa Besodeya; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake. 7#Yos 9:3; Neh 2:8Na baada yao wakafanyiza Melatia, Mgibeoni, na Yadoni, Mmeronothi, watu wa Gibeoni, na wa Mispa, raia wa kiti cha enzi cha liwali wa ng’ambo ya Mto. 8#Neh 12:38Na baada yao akafanyiza Uzieli, mwana wa Harhaya, mmoja wa mafundi wa dhahabu. Na baada yake akafanyiza Hanania, mmoja wa mafundi wa manukato, nao wakaujengea Yerusalemu buruji mpaka ule ukuta mpana. 9Na baada yao akafanyiza Refaya, mwana wa Huri, akida wa nusu ya Yerusalemu. 10Na baada yao akafanyiza Yedaya, mwana wa Harumafu, kuielekea nyumba yake. Na baada yake akafanyiza Hatushi, mwana wa Hashabneya. 11#Ezr 2:32Malkiya, mwana wa Harimu, na Hashubu, mwana wa Pahath-moabu, wakafanyiza sehemu nyingine, na mnara wa tanuu. 12#Kut 35:25; Lk 8:3; Flp 4:3Na baada yake akafanyiza Shalumu, mwana wa Haloheshi, akida wa nusu ya Yerusalemu, yeye na binti zake. 13#Neh 2:13; Yos 15:34Lango la bondeni wakalifanyiza Hanuni, nao wakaao Zanoa; wakalijenga, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake, na huo ukuta wa dhiraa elfu mpaka lango la jaa. 14#Yer 6:1; Mik 1:11Na lango la jaa akalifanyiza Malkiya, mwana wa Rekabu, akida wa mtaa wa Beth-hakeremu; akalijenga, akaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake. 15#Neh 2:14; Yos 18:26; Amu 20:1-3; Yer 40:6; Isa 8:6; Lk 13:4; Yn 9:7Na lango la chemchemi akalifanyiza Shalumu, mwana wa Kolhoze, akida wa mtaa wa Mispa; akalijenga na kulifunika, akaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake, na huo ukuu wa birika la Shiloa karibu na bustani ya mfalme, mpaka madaraja yashukayo kutoka mji wa Daudi. 16#2 Fal 20:20; Isa 22:11; Wim 3:7Baada yake akafanyiza Nehemia, mwana wa Azbuki, akida wa nusu ya mtaa wa Beth-suri, mpaka mahali paelekeapo makaburi ya Daudi, na mpaka birika lililofanyizwa, na mpaka nyumba ya mashujaa. 17Baada yake wakafanyiza Walawi, Rehumi, mwana wa Bani. Baada yake akafanyiza Hashabia, akida wa nusu ya mtaa wa Keila, kwa mtaa wake. 18#Yos 15:44; 1 Sam 23:1Baada yake wakafanyiza ndugu zao, Binui, mwana wa Henadadi, akida wa nusu ya mtaa wa Keila. 19#2 Nya 26:9Na baada yake akafanyiza Ezeri, mwana wa Yeshua, akida wa Mispa, sehemu nyingine, kupaelekea penye kupanda kwa ghala ya silaha, ukuta ugeukapo. 20#Mhu 9:10; Rum 12:11Baada yake Baruki, mwana wa Zakai, akafanyiza kwa bidii sehemu nyingine, toka ugeukapo ukuta mpaka mlango wa nyumba ya Eliashibu, kuhani mkuu. 21Baada yake akafanyiza Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, sehemu nyingine, toka mlango wa nyumba ya Eliashibu mpaka mwisho wa nyumba ya Eliashibu. 22Na baada yake wakafanyiza makuhani, watu wa Uwandani. 23Baada yao wakafanyiza Benyamini na Hashubu, kuielekea nyumba yao. Baada yao akafanyiza Azaria, mwana wa Maaseya, mwana wa Anania, kando ya nyumba yake. 24Baada yake akafanyiza Binui, mwana wa Henadadi, sehemu nyingine, toka nyumba ya Azaria mpaka ugeukapo ukuu, na mpaka pembeni. 25#Neh 12:39; Yer 32:2Baada yake akafanyiza Palali, mwana wa Uzai, kuelekea ugeukapo ukuta, nao mnara utokezao penye nyumba ya juu ya kifalme, iliyopo karibu na uwanda wa walinzi. Baada yake akafanyiza Pedaya, mwana wa Paroshi, 26#Ezr 2:43; Neh 7:46; 8:1-3(basi Wanethini hukaa Ofeli), mpaka mahali paelekeapo lango la maji kukabili mashariki, nao mnara utokezao. 27Baada yake wakafanyiza Watekoi sehemu nyingine, kuuelekea mnara mkubwa utokezao, na mpaka ukuta wa Ofeli. 28#2 Fal 11:16; 2 Nya 23:15; Yer 31:40Juu ya lango la farasi wakafanyiza makuhani, kila mtu kuielekea nyumba yake. Baada yao akafanyiza Sadoki, mwana wa Imeri, kuielekea nyumba yake. 29#Yer 19:2Na baada yake akafanyiza Shemaya, mwana wa Shekania, mlinzi wa lango la mashariki. 30Baada yake wakafanyiza Hanania, mwana wa Shelemia, na Hanuni, mwana wa sita wa Salafu, sehemu nyingine. Baada yake akafanyiza Meshulamu, mwana wa Berekia, sehemu nyingine kuelekea chumba chake. 31Baada yake akafanyiza Malkiya, mmoja wa mafundi wa dhahabu, mpaka nyumba ya Wanethini, na ya wafanya biashara, kulielekea lango la gereza, na mpaka chumba cha juu cha pembeni. 32#Neh 12:39; Yn 5:2Na kati ya chumba cha juu cha pembeni na lango la kondoo wakafanyiza mafundi wa dhahabu na wafanya biashara.

Currently Selected:

Neh 3: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy