YouVersion Logo
Search Icon

Law 2

2
Sadaka za Nafaka
1 # Law 6:14; 9:17 Na mtu atakapomtolea BWANA matoleo ya sadaka ya unga, matoleo yake yatakuwa ya unga mwembamba; naye ataumiminia mafuta, na kutia na ubani juu yake; 2#Law 5:12; 6:15; 24:7; Isa 66:3; Mdo 10:4kisha atauleta kwa wana wa Haruni, hao makuhani; naye atatwaa konzi moja katika huo unga mwembamba, na katika mafuta yake, na huo ubani wote; kisha kuhani atauteketeza kuwa ndio ukumbusho wake juu ya madhabahu, ni kafara ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA; 3#Law 7:9; 10:12,13; Kut 29:37; Hes 18:9na huo uliosalia wa ile sadaka ya unga utakuwa ni wa Haruni na wanawe; ni kitu kitakatifu sana katika sadaka zilizosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.
4 # Kut 29:2 Tena, utakapotoa matoleo ya sadaka ya unga uliookwa tanuuni, yatakuwa mikate isiyotiwa chachu, ya unga mwembamba uliokandwa na mafuta, au maandazi yasiyochachwa yaliyopakwa mafuta. 5Tena matoleo yako kwamba ni sadaka ya unga wa kaangoni, yatakuwa ya unga mwembamba usiotiwa chachu, uliokandwa na mafuta. 6Utaukata-kata vipande, na kutia mafuta juu yake; ni sadaka ya unga. 7Tena matoleo yako kwamba ni sadaka ya unga ya chunguni, yataandaliwa kwa unga mwembamba pamoja na mafuta. 8Nawe utamletea BWANA sadaka ya unga iliyofanywa ya vitu hivyo; nayo italetwa kwa kuhani, naye ndiye atakayeisongeza madhabahuni. 9#Kut 29:18; Rum 12:1Kisha kuhani atatwaa humo huo ukumbusho wa sadaka ya unga, naye atauteketeza juu ya madhabahu; ni kafara ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA. 10#Kut 29:18,37Na hicho kitakachosalia katika sadaka ya unga kitakuwa cha Haruni na wanawe; ni kitu kitakatifu sana katika sadaka zilizosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto. 11#Law 6:17; Mt 16:12; Mk 8:15; Lk 12:1; 1 Kor 5:8; Gal 5:9Sadaka ya unga iwayo yote itakayosongezwa kwa BWANA isitiwe chachu kabisa; kwa kuwa hamtateketeza chachu, wala asali iwayo yote, kuwa ni sadaka ya kusongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto. 12#Kut 22:29; Law 23:10,11; Kum 26:10Vitu hivyo mtavisongeza kwa BWANA kuwa ni malimbuko; lakini visifike juu ya madhabahu kuwa ni harufu ya kupendeza.
13 # Mk 9:49; Kol 4:6; Hes 18:19; Eze 43:24 Tena, kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la Mungu wako; utatoa chumvi pamoja na matoleo yako yote.
14 # Kut 23:19; Mit 3:9; Law 23:10,14; 2 Fal 4:42 Nawe kwamba wamtolea BWANA sadaka ya unga ya malimbuko, utatoa hiyo ngano katika masuke yake iliyochomwa motoni, ngano iliyopondwa ya masuke mabichi, ndiyo utakayoleta kuwa sadaka ya unga ya malimbuko yako. 15Nawe utatia mafuta juu yake, na kuweka ubani juu yake; ni sadaka ya unga. 16Huyo kuhani atauteketeza ukumbusho wake, yaani, sehemu ya ngano iliyopondwa ya hiyo sadaka, na sehemu ya mafuta yake, pamoja na ule ubani wake wote; ni kafara ya kusongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.

Currently Selected:

Law 2: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy