YouVersion Logo
Search Icon

Hab 3

3
Ombi la Nabii
1Sala ya nabii Habakuki.#3:1 iliyoimbwa kwa Shigionothi.
2Ee BWANA, nimesikia habari zako, nami naogopa;
Ee BWANA, fufua kazi yako katikati ya miaka;
Katikati ya miaka tangaza habari yake;
Katika ghadhabu kumbuka rehema.
3Mungu alikuja kutoka Temani,
Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani.
Utukufu wake ukazifunika mbingu,
Nayo dunia ikajaa sifa yake.
4Mwangaza wake ulikuwa kama nuru;
Alikuwa na mishale ya nuru ubavuni pake;
Ndipo ulipofichwa uweza wake.
5Mbele zake ilikwenda tauni,
Na makaa ya moto yakatoka miguuni pake.
6 # Kut 23:31; Kum 32:8; Hes 21:24,34 Akasimama, akaitetemesha dunia;
Akatazama, akawasitusha mataifa;
Na milima ya zamani ikatawanyika;
Vilima vya kale vikainama;
Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.
7Naliziona hema za Kushani katika taabu;
Mapazia ya nchi ya Midiani yakatetemeka.
8 # Kut 14:21,22 Je! BWANA aliikasirikia mito?
Je! Hasira yako ilikuwa juu ya mito,
Au ghadhabu yako juu ya bahari,
Hata ukapanda farasi zako,
Katika magari yako ya wokovu?
9Uta wako ukafanywa wazi kabisa;
Viapo walivyopewa kabila vilikuwa neno thabiti;
Ukaipasua nchi kwa mito.
10Milima ilikuona, ikaogopa;
Gharika ya maji ikapita;
Vilindi vikatoa sauti yake,
Vikainua juu mikono yake.
11Jua na mwezi vikasimama makaoni mwao;
Mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa,
Mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao.
12 # Zab 44:2,3; Mik 4:13 Ulikwenda katikati ya nchi kwa ghadhabu;
Ukawapura mataifa kwa hasira.
13 # 2 Sam 5:20 Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako,
Kwa ajili ya wokovu wa masihi#3:13 Au, mtiwa mafuta (taz. 1 Sam 2:10). wako;
Ukakiponda kichwa cha nyumba ya waovu,
Ukiuweka wazi msingi hata mwambani.
14Ukakichoma kichwa cha mashujaa wake kwa fimbo zao wenyewe;
Wakaja kama kisulisuli ili kunitawanya;
Kama wakifurahi kuwameza maskini kwa siri.
15Ukaikanyaga bahari kwa farasi zako,
Chungu ya maji yenye nguvu.
16Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka,
Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile;
Ubovu ukaingia mifupani mwangu,
Nikatetemeka katika mahali pangu;
Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki,
Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu.
Imani na Shangwe katika Shida
17 # 2 Kor 4:8,9 Maana mtini hautachanua maua,
Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda;
Taabu ya mzeituni itakuwa bure,
Na mashamba hayatatoa chakula;
Zizini hamtakuwa na kundi,
Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe;
18 # Zab 42:5; Isa 61:10 Walakini nitamfurahia BWANA
Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.
19 # 2 Sam 22:34; Zab 18:33; 27:1 YEHOVA, aliye BWANA, ni nguvu zangu,
Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu,
Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.#3:19 Na apewe mwimbishaji mkuu kwa vinanda vyangu vyenye nyuzi.

Currently Selected:

Hab 3: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy