YouVersion Logo
Search Icon

1 Sam 2

2
Ombi la Hana
1 # Lk 1:46-55; Flp 4:6; Zab 9:14; 13:5; 20:5 Naye Hana akaomba, akasema,
Moyo wangu wamshangilia BWANA,
Pembe yangu imetukuka katika BWANA,
Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu;
Kwa kuwa naufurahia wokovu wako;
2 # Kut 15:11; Isa 6:3; 57:15; Kum 4:35; Zab 73:25 Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA;
Kwa maana hakuna ye yote ila wewe,
Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.
3 # Mal 3:13 Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo;
Majivuno yasitoke vinywani mwenu;
Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa,
Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.
4Pinde zao mashujaa zimevunjika,
Na hao waliojikwaa wamefungiwa nguvu.
5 # Lk 1:53; Zab 113:9; Isa 54:1; Gal 4:27 Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula,
Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha.
Naam, huyo aliyekua tasa amezaa watoto saba,
Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika.
6 # Kum 32:39; Ayu 5:18; Hos 6:1; Yn 5:25-29; 11:25,26; Ufu 1:18 BWANA huua, naye hufanya kuwa hai;
Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.
7 # Ayu 1:21; 5:11; Zab 102:10; 75:7 BWANA hufukarisha mtu, naye hutajirisha;
Hushusha chini, tena huinua juu.
8 # Dan 4:17; Mwa 41:14; 1 Sam 15:17; Ayu 36:7; Yak 2:5; Ufu 1:6; 3:21; Ebr 1:3 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Humpandisha mhitaji kutoka jaani,
Ili awaketishe pamoja na wakuu,
Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu;
Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA,
Naye ameuweka ulimwengu juu yake.
9 # Zab 91:11; 1 Sam 14:6 Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake;
Bali waovu watanyamazishwa gizani,
Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;
10 # Zab 96:13 Washindanao na BWANA watapondwa kabisa;
Toka mbinguni yeye atawapigia radi;
BWANA ataihukumu miisho ya dunia;
Naye atampa mfalme wake nguvu,
Na kuitukuza pembe ya masihi#2:10 Neno hili masihi, kwa Kiebrania, maana yake ni Mtiwa mafuta, au, Mwenye kuwekwa wakfu kwa kutiwa mafuta ili awe mfalme, au kuhani, au nabii. Kwa Kiyunani ni Kristo. wake.
Utovu wa Wana wa Eli
11 # 1 Sam 3:1 Kisha Elkana akaenda Rama nyumbani kwake. Na yule mtoto akamtumikia BWANA mbele yake Eli, kuhani.
12 # Kum 13:13; Rum 1:28 Basi, hao wana wa Eli walikuwa watu wasiofaa kitu; hawakumjali BWANA, 13wala haki ya makuhani ilivyokuwa kwa watu. Wakati huo mtu ye yote alipotoa dhabihu wakati wo wote, ndipo huja mtumishi wa kuhani, nyama ilipokuwa katika kutokota, naye akawa na uma wa meno matatu mkononi mwake; 14naye huutia kwa nguvu humo chunguni, au birikani, au sufuriani, au chomboni; nyama yote iliyoinuliwa kwa huo uma kuhani huichukua mwenyewe. Ndivyo walivyofanya huko Shilo kwa Waisraeli wote waliokuja huko. 15Tena, kabla ya kuteketeza mafuta, huja mtumishi wa kuhani, akamwambia yule mwenye kuitoa dhabihu, Mtolee kuhani nyama ya kuoka; kwa kuwa hataki kupewa nyama iliyotokoswa, bali nyama mbichi. 16Tena, ikiwa mtu yule amwambia, Hawakosi wataichoma moto hayo mafuta kwanza, kisha utwae kadiri roho yako itakavyopenda; ndipo husema, Sivyo, lakini sharti unipe sasa hivi; la, hunipi, basi nitaitwaa kwa nguvu. 17#Mwa 6:11; Mal 2:8; Rum 2:24Hivyo dhambi yao wale vijana ilikuwa kubwa sana machoni pa BWANA; kwa maana hao watu walidharau sadaka ya BWANA.
Mtoto Samweli akiwa Shilo
18 # Kut 28:4 Lakini Samweli alikuwa akitumika mbele za BWANA, naye alikuwa kijana, mwenye kuvaa naivera ya kitani. 19Tena mamaye humfanyizia kanzu ndogo, na kumletea mwaka kwa mwaka, hapo alipokwea pamoja na mumewe ili kutoa dhabihu kila mwaka. 20Naye Eli akambariki Elkana na mkewe, akasema, BWANA na akupe uzao kwa mwanamke huyu, badala ya azimo aliloazimiwa BWANA. Kisha wakaenda nyumbani kwao. 21#Mwa 21:1; Lk 2:40Naye BWANA akamwangalia Hana, naye akachukua mimba, akazaa watoto, wa kiume watatu na wa kike wawili. Naye huyo mtoto Samweli akakua mbele za BWANA.
Unabii dhidi ya Nyumba ya Eli
22Basi Eli alikuwa mzee sana; naye alisikia habari za mambo yote ambayo wanawe waliwatenda Waisraeli; na jinsi walivyolala na wanawake waliokuwa wakitumika mlangoni pa hema ya kukutania. 23Akawaambia, Mbona mnatenda mambo kama hayo? Maana nasikia habari za matendo yenu mabaya kwa watu hawa wote. 24Sivyo hivyo, wanangu, kwa maana habari hii ninayoisikia si habari njema; mnawakosesha watu wa BWANA. 25#Hes 15:30; Kum 2:30; Mit 15:10; Yn 12:39,40Mtu mmoja akimkosa mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosa BWANA, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwa sababu BWANA amekusudia kuwaua. 26#Lk 2:52; Mit 3:4; Lk 2:40; Mdo 2:47; Rum 14:18Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa BWANA, na kwa watu pia.
27 # 1 Fal 13:1; Kut 4:14 Kisha mtu wa Mungu akamwendea Eli, akamwambia, BWANA asema hivi, Je! Mimi sikujidhihirisha nafsi yangu kwa nyumba ya baba yako, walipokuwa katika Misri, wakiitumikia nyumba ya Farao? 28#Kut 28:1-4; Law 7:35-36; 2:3Je! Sikumchagua yeye katika kabila zote za Israeli, ili awe kuhani wangu, apande madhabahuni kwangu; na kufukiza uvumba, na kuvaa naivera mbele zangu? Nami sikuwapa watu wa mbari ya baba yako dhabihu zote za wana wa Israeli zilizotolewa kwa moto? 29#Kum 32:15; Mal 1:12; Kum 12:5Kwa nini basi mnaipiga teke dhabihu yangu na sadaka yangu nilizoziamuru katika maskani yangu; ukawaheshimu wanao kuliko mimi, mpate kujinenepesha kwa sadaka zote za watu wangu Israeli zilizo njema? 30#1 Nya 15:2; Yer 18:9; Zab 18:20; 91:14; Yn 5:44; 12:26; 1 Pet 1:7; Hes 11:20; 2 Sam 12:9,10; Mal 2:9Kwa sababu hiyo, BWANA, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa BWANA asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu. 31#1 Sam 4:11Angalia, siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa mbari ya baba yako, hata nyumbani mwako hatakuwako mzee. 32#Zek 8:4Nawe utalitazama teso la maskani yangu, katika utajiri wote watakaopewa Israeli; wala nyumbani mwako hatakuwako mzee milele. 33Tena mtu wa kwako, ambaye sitamtenga na madhabahu yangu, atakuwa mtu wa kukupofusha macho, na kukuhuzunisha moyo; tena wazao wote wa nyumba yako watakufa wapatapo kuwa watu wazima. 34#1 Sam 4:11Na hii ndiyo ishara itakayokuwa kwako, itakayowapata wana wako wawili, Hofni na Finehasi; watakufa wote wawili katika siku moja. 35#1 Fal 2:35; 1 Nya 29:22; Ebr 2:17; 7:26-28; 2 Sam 7:11; 1 Fal 11:38; Zab 2:2Nami nitajiinulia kuhani mwaminifu, atakayefanya sawasawa na mambo yote niliyo nayo katika moyo wangu, na katika nia yangu; nami nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi#2:35 Au, mtiwa mafuta (taz. 1 Sam. 2:10). wangu milele. 36#1 Fal 2:27Kisha itakuwa, ya kwamba kila mtu atakayesalia katika nyumba yako atakwenda kumsujudia, apate kipande kidogo cha fedha, na mkate mmoja; na kumwambia, Tafadhali unitie katika kazi mojawapo ya ukuhani, nipate kula kipande kidogo cha mkate.

Currently Selected:

1 Sam 2: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy