Warumi 5:1-2
Warumi 5:1-2 TKU
Tumehesabiwa haki mbele za Mungu kwa njia ya imani. Hivyo sote tuna amani pamoja na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. Kupitia imani yetu, Kristo ametufungulia mlango kuingia katika neema ya Mungu, tunayoifurahia sasa. Na tunashangilia sana kwa sababu ya tumaini tulilonalo la kushiriki utukufu wa Mungu.




