Warumi 10:11-13

Warumi 10:11-13 TKU

Ndiyo, Maandiko yanasema, “Yeyote anayemwamini hataaibika.” Yanasema hivi kwa sababu hakuna tofauti kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi. Bwana yule yule ndiye Bwana wa watu wote. Naye humbariki sana kila amwombaye akitaka msaada. Ndiyo, “kila mtu anayemwita Bwana ili kupata msaada, ataokolewa.”