YouVersion 標識
搜索圖示

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA NANE預覽

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA NANE

7天中的第4天

  

MWANAMKE ALIYEFUMANIWA AKIZINI

Lakini Yesu akaenda katika Mlima wa Mizeituni.

Alfajiri na mapema Yesu akaja tena Hekaluni, watu wote wakakusanyika, akakaa akaanza kuwafundisha.

"Walimu wa sheria na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya umati wa watu wote.Wakamwambia Yesu,"

"“Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini.Katika sheria, Mose alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake wa namna hii, mpaka wafe. Sasa wewe wasemaje?”"

Walimwuliza swali hili kama mtego ili wapate sababu ya kumshtaki.

Lakini Yesu akainama akaanza kuandika ardhini kwa kidole chake.Walipoendelea kumwulizauliza akainuka, akawaambia, 

“Kama kuna mtu ye yote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe.”

Akainama tena na kuandika ardhini.

Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, wakianzia wazee, hadi Yesu akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama mbele yake.

Yesu akainuka na kumwambia, “Wako wapi wale waliokuwa wanakuhukumu kuwa mwenye hatia?”

Yule mwanamke akajibu, “Hakuna hata mmoja Bwana.”

Yesu akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Nenda zako, kuanzia sasa usitende dhambi tena.”

關於此計劃

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA NANE

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana

More

相關題材的計畫