Soma Biblia Kila Siku 04/2025预览

Kufuata maagizo ya Bwana huleta baraka.Haruni akainua mikono yake na kuielekeza kwa hao watu, akawabariki; kisha akashuka akisha isongeza sadaka ya dhambi, na sadaka ya kuteketezwa, na sadaka za amani(9:22). Kufanya kinyume na maagizo hayo huleta kifo. Kuhusu ile sadaka iliyosababisha kifo cha wana wawili wa Haruni, tunajua tu kwamba Bwana hajaiagiza. Habari ya “motowa kigeni” inaeleza tu jinsi walivyomtolea uvumba, siyo kwamba shida ilikuwa kwenye moto. Ndugu uliyeitwa na Bwana kuitangaza Injili, usiyategemee mawazo yako. Hebu jiulize kama unatumika kwa kumtegemea Bwana na maagizo yake? Ukifanya kinyume, ujue kazi yako haitakuwa na baraka, bali kifo.
读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More