Soma Biblia Kila Siku 09/2024预览

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

30天中的第1天

Kukamatwa kwa Yesu na hatimaye kuuawa halikuwa jambo lililotokana na uhodari wa wakuu wa makuhani na viongozi wengine. Yesu mwenyewe aliyajua yote yaliyompata, na hata akawaambia wanafunzi wake ili wasije wakafadhaika na kukata tamaa wakati wa kifo chake. Habari hii inatupa ushuhuda kwamba, mpango mzima wa kuja kwa Yesu duniani, kufa na hata kufufuka kwake, uliratibiwa mbinguni. Hatuna sababu ya mashaka kuhusu ukombozi mkamilifu pale msalabani, kwani ni mpango wa Mungu.

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More