Soma Biblia Kila Siku 08/2024预览

Soma Biblia Kila Siku 08/2024

31天中的第4天

Yosia, Mfalme wa Yuda, aliyaondoa machukizo yote yaliyokuwa ndani ya Yuda. Hapa katika m.24 wanatajwa wenye pepo wa utambuzi, wachawi, vinyago na sanamu zilizokuwa katika Yuda wakati huo:Wenye pepo wa utambuzi, na wachawi, na vinyago, na sanamu, na machukizo yote yaliyoonekana katika nchi ya Yuda na katika Yerusalemu, Yosia akayaondoa yote, ili apate kuyathibitisha maneno ya torati yaliyoandikwa katika kile kitabu alichokiona Hilkia kuhani ndani ya nyumba ya Bwana. Cha ajabu ni kwamba makuhani sio wanaoshughulika na kurudisha ibada za Bwana kwenye utakatifu wake, bali Mfalme Yosia. Ni baraka ya nchi watu wa serikali na kanisa wanaposaidiana kuleta ibada za kweli. Mungu anaweza kukutumia hata wewe kwa utumishi wake. Umruhusu akutakase na akutumie atakavyo.

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 08/2024

Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu

More