Soma Biblia Kila Siku 08/2024预览

Soma Biblia Kila Siku 08/2024

31天中的第13天

Neema ya Mungu ni kuu katika maisha yetu. Tafakari tu jinsi ilivyodhihirishwa katika maisha ya Paulo. Aliwatesa sana wale waliomhubiri Yesu kama mwokozi. Lakini akiwa njiani kwenda Dameski kuwatesa watu wa Mungu alikutana na Yesu Kristo, akabatizwa na maisha yake yakabadilika, akawa mtume wa Bwana wake mpya. Neema ya Mungu ni kuu kuliko ubaya wetu, kama Paulo mwenyewe anavyojumlisha matukio yote katika maisha yake:Neema ya Bwana wetu ilizidi sana, pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu(m.14). Hata kama unahisi wewe ni mbaya kuliko watu wote, umgeukie Yesu. Yeye anaweza kukubadilisha uwe mtumishi wake mwema kama Paulo.

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 08/2024

Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu

More