Soma Biblia Kila Siku 06/2024预览

Kuna msemo usemao, "Woga ni muuaji wa kila maono mema". Kwa hiyo Paulo anamkumbusha Timotheo asiangukie katika roho ya woga. Je, umewahi kufikiria jinsi mtu mwoga anavyoweza kumshuhudia Kristo Yesu? Ni vigumu, sivyo! Kwa hiyo tumshukuru Bwana wetu kwamba hajatuacha hivi hivi tulivyo, bali amewapa waaminio Roho wake wa nguvu, upendo na kiasi. Roho Mtakatifu ndiye anayewahakikisha wasioamini na kutupa kujivunia Injili, kwani niuweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye(Rum 1:16).
读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More