Soma Biblia Kila Siku 05/2024预览

Soma Biblia Kila Siku 05/2024

31天中的第25天

Matakwa ya wana wa Israeli yalimfanya Haruni amwasi Mungu na kujivunjia heshima ya utumishi wake mtakatifu. Kama Haruni angelikataa wazo la watu, taifa zima lisingelitenda uovu ule. Viongozi, wawe wa kanisa ama serikali, wajilinde wasiwasikilize watu kuliko Mungu, ili wasiwe sababu ya kanisa na taifa kutenda dhambi. Musa alitaka kujitoa ili Waisraeli wasamehewe. Katika m.31-32 anaomba:Aa! watu hawa wametenda dhambi kuu, wamejifanyia miungu ya dhahabu. Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao – na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika. Lakini uovu wa mtu, familia, kanisa na taifa hausamehewi na kiongozi wa kidini, bali kwa kuomba msamaha kwa Yesu!

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 05/2024

Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More