Soma Biblia Kila Siku 02/2024预览

Soma Biblia Kila Siku 02/2024

29天中的第17天

Kwenye msingi wa agano wawakilishi wa Israeli wanapata kumwona Mungu na kula pamoja naye;naye hakuweka mkono wake juu ya hao wakuu wa wana wa Israeli(m.11). Lakini kuishi na Mungu aliye kama moto uteketezao, kunahitaji utaratibu, na Mungu mwenyewe ndiye anayechukua jukumu hili:Njoo huku juu kwangu mlimani(m.12). Je, unajua Mungu amefanya nini ili kukutana na wewe na mimi? Hatuamriwi kwenda mlimani. Mungu amemtuma Yesu!Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana(Ebr 1:1-2). Na Yesu anasema,Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha(Mt 11:28). Ni upendo, huruma na wema wa Mungu kwamba Yeye aliye Mtakatifu anatualika sisi wenye dhambi kwenda kwake!

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 02/2024

Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu

More