Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021预览

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

31天中的第29天

Sehemu hii inahusu hukumu ya Mungu inayogusa uumbaji wote. Baragumu linalopigwa lina madhumuni yafuatayo: 1. Kuonya kwamba hukumu ipo na ina uhakika. 2. Kuleta nguvu za wema katika mapambano na uovu. 3. Kutangaza kurudi kwa mfalme (Kristo). Maonyo haya yanatupa changamoto ya kujiimarisha. Kuhakikisha kuwa imani yetu imejengwa na kuimarishwa na Kristo mwenyewe. Hukumu ya Mungu inatisha mno. Usipomwamini Kristo hukwepi hukumu hii iliyopo na inayokuja. Mgeukie Kristo sasa.

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.

More