Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021预览

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

31天中的第13天

Daudi kukosa msimamo mbele ya wana wake kulionekana tena kabla hawajaanza vita hii. Maana aliwaagiza na kuwasisitizia wasimwue Absalomu (m.5, Mtendeeni yule kijana, Absalomu, kwa upole kwa ajili yangu), ingawa ni wazi kabisa kwamba Absalomu ni adui yake aliyekusudia kumwua. Tena alikuwa amelala na masuria ya Daudi. Kisheria adhabu yake ilikuwa ni kifo. Yoabu alitambua wazi mambo haya, kwa hiyo aliamua kumwua Absalomu kinyume cha agizo la mfalme. Alitaka kuliokoa taifa la Mungu. "Vyemba" ni mikuki; na "moyoni", tafsiri yake halisi ni "kifuani" (m.14).

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.

More