Soma Biblia Kila Siku Juni 2021预览

Tunaonyeshwa uharibifu mkubwa utakaoujia Tiro. Mali, utajiri, wataalamu wote, wanajeshi, na sekta zote za weledi wa mji huu, vitu hivi vyote vitateketea, na Tiro utakuwa kitu cha kutisha. Sababu yake imefafanuliwa namna hii: Moyo wako umeinuka, nawe umesema, Mimi ni Mungu, nami nimeketi katika kiti cha Mungu … … una hekima kuliko Danieli (28:2-3). Kiburi cha kujifanya kuwa Mungu na kujihesabia hekima zaidi ya Danieli, ni kosa liletalo hukumu na kifo. Utabiri na maombolezo haya kwa Tiro yalitegemewa kuleta toba, kama Ninive ilivyoonywa kwa ujumbe wa Yona. Inatupasa nasi leo tuzitafakari njia zetu na kutubu zilizo mbaya.
读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More